• HABARI MPYA

    Thursday, May 21, 2026

    JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA FOUNTAIN GATE, 2-2 MBWENI


    WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na winga Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 53 na mshambuliaji Paul Peter Kasunda dakika ya 86, wakati ya Fountain Gate yamefungwa na winga wa kulia, Juma Issa Abushiri 'Messi wa Chuga' dakika ya tatu na kiungo Ismail Aziz Kader dakika ya 45.
    Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya sita na Fountain Gate inafikisha pointi 26 nayo inabaki nafasi ya 11 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 24 kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.   

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA FOUNTAIN GATE, 2-2 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top