• HABARI MPYA

  Monday, July 18, 2016

  ZIDANE AZINGUANA NA RAIS REAL MADRID KISA KINDA LA NORWAY ODEGAARD

  KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametofautiana na Rais wa klabu juu ya kinda wa umri wa miaka 17, Martin Odegaard.
  Zidane hakutaka kumchukua kiungo huyo kinda katika ziara ya kujiandaa na msimu nchini Canada, lakini Florentino Perez akasema huo ni ukiukwaji mkubwa wa kwanza wa makubaliano tangu Zidane aanze kazi Januari.
  Perez anataka Odegaard aijumuishwe kwenye ziara kwa sababu katika Mkataba wake kua kipengele cha kujumuishwa katika kikosi cha kwanza na kwa sababu pia ushiriki wake katika mechi za Amerika Kusini utasaidia kumpatia timu mpya kipindi hiki cha usajili.
  Pamoja na Zidane kukubali mchezaji huyo atolewe kwa mkopo msimu huu, alipingana na wazo la kuungana nao kwenye ziara hiyo wakati hayupo kwenye mipango yao ya msimu ujao.

  Kocha Zinedine Zidane akijiandaa kupanda basi na wachezaji wake wa Real Madrid mjini Montreal tayari kuanza ziara yao ya kujiandaa na msimu  PICHA ZAIDI GONGA HAPA   


  KIKOSI  CHA REAL MADRID ZIARANI

  Makipa: Navas, Casilla, Ruben Yanez, Craninx, Luca Zidane
  Mabeki: Varane, Danilo, Carvajal, Marcelo, Nacho, Lienhart, Tejero, Achraf
  Viungo: Casemiro, Isco, Kovacic, Llorente, Asensio, Odegaard, Enzo, Febas
  Washambuliaji: Benzema, Jese, Mayoral, Mariano
  ------------- 
  Ratiba: Julai 28 na PSG (Ohio), Julai 30 na Chelsea (Michigan), Agosti 3 na Bayern Munich (New Jersey)
  Hamburg imeonyesha dhamira ya kumsajili Odegaard ahamie Bundesliga msimu ujao na Liverpool - ni moja ya klabu ambazo alikataa kujiunga nazo wakati anaamua kujiunga na Madrid - pia imehusishwa kumtaka tena. 
  Lakini Real inaweza kuchagua kumpeleka klabu nyingine ya Hispania na inataka kuzuia mpango wa klabu hizo kumtwaa kwa kumhusisha Odegaard kwenye mechi ya Super Cup ya Ulaya Agosti 9, mwaka huu kwa sababu itachezwa nchini kwao, Norway.
  Madrid ilimsajili Odegaard Januari mwaka 2015, lakini matumaini kwamba angekomaa haraka na kupata nafasi kikosi cha kwanza yamefifia kutokana na kutofanya vizuri sana katika kikosi cha pili cha klabu, maarufu kama Castilla B ambayo awali ilikuwa inafundishwa na Zidane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE AZINGUANA NA RAIS REAL MADRID KISA KINDA LA NORWAY ODEGAARD Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top