• HABARI MPYA

    Tuesday, July 19, 2016

    YANGA NA AZAM AGOSTI 17 NGAO YA JAMII, SIMBA KUFUNGUA DIMBA NA NDANDA LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa mataji yote nchini, Yanga SC watamenyana na washindi wa pili wa mashindano yote, Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyovuja na kuifikia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE, Yanga watafungua dimba na JKT Ruvu Agosti 31 Uwanja wa Taifa.
    Kwa ujumla Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/ 2017 itaanza Agosti 20, Simba SC wakifungua dimba na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Beki wa Yanga, Kevin Yondan akimiliki mpira pembeni ya mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (kulia)
    Mechi nyingine za ufunguzi zitakuwa kati ya Kagera Sugar na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Toto Africans na Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United na Mbao FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji Songea.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA AZAM AGOSTI 17 NGAO YA JAMII, SIMBA KUFUNGUA DIMBA NA NDANDA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top