• HABARI MPYA

    Wednesday, July 20, 2016

    TFF KUTUMIA FEDHA ZA MECHI YA NGAO KUNUNULIA MADAWATI 200

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato ya Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 17, 2016.
    TFF inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na juhudi za Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.
    Kadhalika TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah kwa juhudi za kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika kuliletea Taifa maendeleo.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amewataka makocha 20 wanaoshiriki kozi ya ukocha wa leseni A, kwenda kutumia elimu hiyo kusaidia na kuendeleza soka katika nyanja mbalimbali

    TFF itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports Club katika kufanikisha mashindano mbalimbali hasa mchezo wa Hisani kati ya Simba Sports Club na Young African (Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.
    Wakati huo huo: Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amewataka makocha 20 wanaoshiriki kozi ya ukocha wa leseni A, kwenda kutumia elimu hiyo kusaidia na kuendeleza soka katika nyanja mbalimbali.
    Malinzi aliyasema hayo jana Julai 19, 2016 wakati akifungua kozi hiyo ambayo inashirikisha makocha 20 na kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    “Ndugu zangu makocha nawasihi mnapohitimu kozi hii msiende kuweka vyeti vyenu ndani bali mkawe chachu ya mafanikio ya soka kwani kwa idadi ya makocha 23 ambao wana leseni A ni makocha saba tu ambao wanafundisha,” alisema Malinzi.
    Pia Malinzi alisema ikimaliza kozi hii Tanzania itakuwa na makocha 43 wenye leseni A jambo ambalo ni idadi ndogo ikilinganishwa na Tanzania ambayo ina watanzania milioni 50.
    Pia Malinzi alisema kuanzia msimu huu mpya wa ligi makocha watakaoruhusiwa kuwa na timu za ligi kuu ni wale wenye leseni A na kwa daraja la kwanza ni wenye leseni B huku akisema wasaidizi watatakiwa kuwa na leseni C.
    Kozi hii itakuwa inafendeshwa na mkufunzi Sunday Kayuni akisaidia na Salum Madadi na itakuwa ya mwezi mmoja lakini ikimalizika wiki mbili itasimama na kuja kumalizika baadaye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF KUTUMIA FEDHA ZA MECHI YA NGAO KUNUNULIA MADAWATI 200 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top