• HABARI MPYA

    Friday, July 15, 2016

    SAMATTA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO EUROPA LEAGUE GENK IKIUA 2-0

    Na Mwandishi Wetu, GENK
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga bao lake la kwanza katika michuano ya Europa League usiku huu, timu yake, KRC Genk ikiilaza 2-0 Buducnost ya Montenegro Uwanja wa  Luminus Arena mjini Genk.
    Katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya mchujo, Samatta alifunga bao la pili dakika ya 79, baada ya kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Neeskens Kebano kufunga la kwanza kwa penalti dakika ya 16.  
    Genk sasa itatakiwa kwenda kuulinda ushindi wake katika mchezo wa marudiano Julai 21, Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica ili kusonga mbele Raundi ya Tatu ya mchujo.
    Samatta (wa pili kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga
    Ratiba ya Raundi ya Tatu ya mchujo itapangwa leo na mechi za kwanza zitachezwa Julai 28 wakati marudiano yatakuwa Agosti 4, mwaka huu.
    Timu zitakazoshinda zitakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi, ambako sasa vigogo kama Manchester United ya England wataanzia huko.
    Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Castagne, Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Buyens/Heynen dk73, Kebano/Karelis dk76, Bailey, Buffalo na Samatta/Trossard dk87.
    Buducnost Podgorica : Dragojevic, Vusurovic (84 'Camaj), Mitrovic, Vukcevic, Radunović, Pejakovic/Seratlic dk74 Raickovic/Janketić dk59, Hoko, Đalović, Mirkovic na Raspopovic
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO EUROPA LEAGUE GENK IKIUA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top