• HABARI MPYA

  Sunday, July 17, 2016

  RODRIGUEZ AANZA NA DOZI YA 2-0 KIRAFIKI AZAM FC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KOCHA mpya wa Azam FC, Mspaniola Zeben Hernandez Rodriguez ameanza kwa ushindi wa mabao 2-0 asubuhi ya leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ashanti United ya Daraja la Kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kiungo Mudathir Yahya alianza kuwafungia washindi hao wa Medali za Fedha za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) dakika ya 69 kwa shuti la kiufundi kufuatia pasi ya kiungo Frank Domayo.
  Mudathir Yahya (kulia) amefunga bao moja Azam FC ikishinda 2-0 asubuhi ya leo
  Na Abdallah Masoud 'Cabaye' akawafungia bao la pili dakika ya 81 mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa shuti zuri la umbali wa mita 30.
  Kocha Rodriguez alipanga vikosi viwili tofauti kipindi cha kwanza akiwaanzisha Juan Jesus Gonzalez, Wazir Salum, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Bolou, Jean Mugiraneza, Ramadhani Singano 'Messi', Ibrahima Fofana, Shaaban Idd na Salum Abubakar 'Sure Boy' ambao wote aliwatoa kipindi cha pili na kuingiza wengine. 
  Kikosi cha Azam kilikuwa; Juan Jesus Gonzalez/Aishi Manula dk 46, Wazir Salum/Gadiel Michael dk 46, Erasto Nyoni/Abdallah Kheri dk 46, Aggrey Morris/Ismail Gambo dk 46, David Mwantika/Himid Mao dk 46, Michael Bolou/Frank Domayo dk 46, Jean Mugiraneza/Mudathir Yahya dk 46/Himid Mao dk 77, Salum Abubakar/ Abdallah Masoud ‘Cabaye’ dk 46, Ramadhan Singano/Khamis Mcha dk 46, Ibrahima Fofana/Kelvin Friday dk 46, Shaaban Idd/AmeAlly dk 46.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RODRIGUEZ AANZA NA DOZI YA 2-0 KIRAFIKI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top