• HABARI MPYA

  Monday, July 18, 2016

  MBEYA CITY YAZIDI KUJIIMARISHA, YASAJILI BEKI LA YANGA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  BEKI wa kati Rajab Zahir aliyekuwa akicheza kwa mkopo Stand United kutoka  Yanga SC ya Dar es Salaam amejiunga na Mbeya City FC leo.
  Kwenye ofisi za City zilizopo Mkapa Hall, eneo la Soko Matola mjini hapa, Zahir amesaini Mkataba wa mwaka mmoja kujunga na  kikosi cha kocha Mmalawi Kinnah Phiri na kusema kwamba ana imani kubwa ya kupata mafanikio yake  kisoka akiwa na chini ya kocha  huyo bora barani.
  “Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kujiunga na City, hii ni moja kati ya timu kubwa nchini kwa sababu ina ushawishi wa kutosha  kwenye soka la nchini yetu, kitu muhimu ni kuomba ushirikiano kutoka kwa pande zote  kwa maana ya uongozi wachezaji wenzangu na mashabiki,  hayo yote yatatufanya kutimiza malengo kwa sababu  kila mmoja anahitaji mafanikio katika kazi  kwangu mimi hapa ndiyo sehemu  ambayo nitayapata” alisema. 
  Rajab Zahir akiwa na jezi ya Mbeya City baada ya kusaini leo
  Zahir amejiunga na City baada ya msimu mmoja wa mkopo kwa Stand  United ya  Shinyanga  uliohitimisha kandarasi yake ya miaka mitatu na kikosi cha  Yanga ya Dar es Salaam.
  Akiwa Stand United, Zahir alifanikiwa kucheza michezo 23 katika mechi zote 30 zilizochezwa na timu hiyo ya Shinyanga na kufanikiwa kushika nafasi ya 7 ikikusanya jumla ya pointi 40 mwisho wa msimu  uliopita.
  Wakati huo huo: Mbeya City FC imekwenda kuweka kambi Kyela kwa siku 10 kabla ya kuhamia Malawi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAZIDI KUJIIMARISHA, YASAJILI BEKI LA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top