• HABARI MPYA

  Sunday, July 17, 2016

  MAHAKAMA MISRI YAMUACHIA HOSSAN LICHA YA KUMPIGA MPIGA PICHA

  MAHAKAMA nchini Misri imemuachia huru gwiji wa soka nchini humo na kocha wa Al-Masry, Hossam Hassan jana baada ya kumpiga mpiga picha na kumharibia kamera yake uwanjani.
  Akiwa mchezaji, Hassan, mwenye umri wa miaka 49 sasa, aliisaidia Misri kutwaa mataji matatu ya Kombe la Mataifa ya Afrika akiwafungia Mafarao jumla ya mabao 69 katika mechi 176 na alifahamika pia kwa hasira zake ugomvi uwanjani.
  Hassan alilipa faini ya Pauni 500 za Misri sawa na dola za Kimarekani 56 na kuruhusiwa kutoka gereza la Tora, Cairo jana.
  Kocha wa Al-Masry, Hossam Hassan ameachiwa huru jana baada ya kumpiga mpiga picha na kumharibia kamera yake uwanjani

  Alikamatwa baada ya kumuangusha chini na kumpiga mpiga picha aliyekuwa anapiga picha baada ya kutokea ugomvi wa wachezaji Al-Masry, timu ya Port Said team Hassan ikitoka sare ya 2-2 na Ghazl el-Mahalla wiki iliyopita.
  Jana Shirikisho la Soka Misri lilimfungia mechi tatu Hassan na kumtoza faini ya Pauni 10,000 za Misri, sawa na dola za Kimarekani 1,100).
  Klabu yake pia ilipigwa faini ya Pauni 20,000 za Misri sawa na dola za Kimarekani 2,200.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAHAKAMA MISRI YAMUACHIA HOSSAN LICHA YA KUMPIGA MPIGA PICHA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top