• HABARI MPYA

  Thursday, July 14, 2016

  BANGOURA AWABWAGA WAZUNGU 'MATAWI YA JUU' UKOCHA WA GUINEA

  SHIRIKISHO la Soka Guinea limemteua kocha wake wa muda, Mohamed Kanfory Bangoura kuwa kocha kamili kuiongoza timu ya taifa ya nchi hiyo katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
  Bangoura, anayefahamika kama Lappe Bangoura, alichaguliwa mbele ya makocha wa thamani ya juu, Mbelgiji Paul Put na Mjerumani Gernot Rohr.
  Tangu kuondoka kwa Luis Fernandez Mei timu ya taifa ya Guinea imekuwa ikitafuta kocha wa kuingia naye kwenye Raundi ya pili ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
  Mohamed Kanfory Bangoura amateuliwa kuwa kocha kamili wa timu ya taifa ya Guinea kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018

  Wamepangwa pamoja na Tunisia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Libya katika hatua hiyo ya mwisho ya mchujo wa kwenda Urusi miaka miwili ijayo.
  Pia inakabiliwa na mchezo wa mwisho wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Januari mwakani nchini Gabin dhidi ya Zimbabwe mjini Conakry Septemba 4, mwaka huu.
  Beki wa kati wa Guinea na Saint Etienne, Florentin Pogba, kaka wa kiungo nyota wa Ufaransa, Paul Pogba, ndiye Nahodha wa timu ya taifa ya Guinea. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BANGOURA AWABWAGA WAZUNGU 'MATAWI YA JUU' UKOCHA WA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top