TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Mabao yote ya Singida Big Stars yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya nane na 15, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefungwa na mshambuliaji mzawa, Yasin Mohamedi Mgaza 58.
Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 13, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Yanga ambayo ina mechi mbili mkononi na wote wapo nyuma ya Azam FC yenye pointi 30 za mechi 13 na Simba SC yenye pointi 28 za mechi 11.
Kwa upande wao Dodoma Jiji baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 16 za mechi 14 sasa nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment