MSHAMBULIAJI wa Atalanta ya Italia, Mnigeria, Ademola Lookman ameshinda Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika kwa wanaume.
Lookman amewaangusha Ronwen Williams, kipa Muafrika Kusini wa Mamelodi Sundowns, mshambuliaji, Serhou Guirassy wa Guinea na Borussia Dortmund, Simon Adingra wa Ivory Coast na Brighton & Hove Albion na beki Achraf Hakimi wa Morocco na Paris Saint-Germain.
Anakuwa Mnigeria wa pili mfululizo kushinda Tuzo hiyo baada Victor James Osimhen anayecheza kwa mkopo Galatasaray ya Uturuki kutoka Napoli ya Italia – hii ikiwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kubeba mtawalia Tuzo hiyo tangu kupokezana kwa Nwankwo Kanu (1996) na Victor Ikpeba (1997), karibu miongo mitatu sasa imepita.
Naye mshambuliaji Mzambia, Barbra Banda anayechezea klabu ya Orlando Pride ya Marekani ameshinda Tuzo ya Mwanasioka Bora wa Kike Afrika dhidi ya ndugu wawili wa Malawi, Tabitha na Temwa Chawinga, Sanaa Mssoudy wa Morocco, Chiamaka Nnadozie wa Nigeria.
WASHINDI WOTE TUZO ZA CAF 2024
MWANASOKA BORA WA MWAKA (WANAUME)
Ademola Lookman (Nigeria / Atalanta)
MWANASOKA BORA WA MWAKA (WANAWAKE)
Barbra Banda (Zambia / Orlando Pride)
KIPA BORA WA MWAKA (WANAUME)
Ronwen Williams (South Africa / Mamelodi Sundowns)
KIPA BORA WA MWAKA (WANAWAKE)
Chiamaka Nnadozie (Nigeria / Paris FC)
MCHEZAJI BORA WA MWAKA ANAYECHEZA AFRIKA (WANAUME)
Ronwen Williams (South Africa / Mamelodi Sundowns)
MCHEZAJI BORA WA MWAKA ANAYECHEZA AFRIKA (WANAWAKE)
Sanaâ Mssoudy (Morocco / AS FAR)
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA MWAKA (WANAUME)
Lamine Camara (Senegal / AS Monaco)
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA MWAKA (WANAWAKE)
Doha El Madani (Morocco / AS FAR)
KOCHA BORA WA MWAKA (WANAUME)
Emerse Fae (Cote d’Ivoire)
KOCHA BORA WA MWAKA (WANAWAKE)
Lamia Boumehdi (TP Mazembe)
TIMU BORA YA TAIFA YA MWAKA (WANAUME)
Ivory Coast
TIMU BORA YA TAIFA YA MWAKA (WANAWAKE)
Nigeria
KLABU BORA YA MWAKA (WANAUME)
Al Ahly (Misri)
KLABU BORA YA MWAKA (WANAWAKE)
TP Mazembe (DRC)
REFA BORA WA MWAKA (WANAUME)
Mutaz Ibrahim (Libya)
REFA BORA WA MWAKA (WANAWAKE)
Bouchra Karboubi (Morocco)
REFA BORA MSAIDIZI WA MWAKA (WANAUME)
Elvis Guy Noupue Nguegoue (Cameroon)
REFA BORA MSAIDIZI WA MWAKA (WANAWAKE)
Diana Chikotesha (Zambia)
BAO BORA LA MWAKA
Mabululu (Angola)
0 comments:
Post a Comment