// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KMC YAICHAPA PAMBA 1-0 BAO LA HANCE DAKIKA ZA JIOONII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KMC YAICHAPA PAMBA 1-0 BAO LA HANCE DAKIKA ZA JIOONII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, December 16, 2024

    KMC YAICHAPA PAMBA 1-0 BAO LA HANCE DAKIKA ZA JIOONII


    BAO la dakika ya 88 la beki Hance Masoud Msonga limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa 
    Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 18 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya tisa, wakati Pamba Jiji inabaki na pointi zake 12 nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 14.
    NAYO Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya 48 na beki mzawa, Kennedy Wilson Juma dakika ya 62.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 30 na kupanda nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 14.
    Hali inazidi kuwa mbaya kwa Tanzania Prisons ikibaki na pointi zake 11 za mechi 14 na kushuka kwa nafasi moja zaidi hadi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMC YAICHAPA PAMBA 1-0 BAO LA HANCE DAKIKA ZA JIOONII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top