// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MUKWALA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 5-2 BUKOBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MUKWALA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 5-2 BUKOBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 21, 2024

    MUKWALA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 5-2 BUKOBA


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
    Mabao ya Simba SC yamefungwa na beki Shomari Salum Kapombe dakika ya 13, viungo Muivory Coast Jean Charles Ahoua dakika ya 44, Mkongo Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 53 na mshambuliaji Mganda, Steve Dese Mukwala mawili, dakika ya 66 na 85.
    Kagera Sugar ilipata mabao yake ya kufutia machozi mwishoni mwa mchezo, wakifunga beki Datius Peter dakika ya 79 na kiungo Cleophas Anthony Mkandala dakika ya 90’+3.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na Kocha Rais wa Afrika Kusini, Fadlu Davids inafikisha pointi 34 katika mchezo wa 13 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu mbele ya Azam FC yenye pointi 33 za mechi 15 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 30 za mechi 12.
    Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 11 za mechi 15 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka daraja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUKWALA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 5-2 BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top