WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya nane, wakati Namungo FC inakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza Ligi ya timu 16 ukiwa nafasi ya 13 kwa pointi zake 14.
0 comments:
Post a Comment