MUSTAKABALI wa Yaya Toure katika klabu ya Manchester City upo shaken baada ya wakala wake kuishutumu klabu hiyo bingwa Ligi Kuu England kwa kuidharau siku ya kuzaliwa ya mchezaji huyo.
Kiungo huyo wa Ivory Coast, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake unaomfanya alipwe Pauni 220,000 kwa wiki, imeelezwa amechukiwa na kitendo cha kutotumiwa salamu za kufurahia miaka 31 ya kuzaliwa kwake.
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amesema: "Kuna uwezekano mkubwa Yaya akaondoka majira haya ya joto. Amechukizwa. Kilichotokea katika birthday take kinamaanisha klabu haimjali. Imethibitika,"amesema.
Maneno mazito: Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amesema kuna uwezekano kiungo huyo akaondoka Etihad
"Katika timu ya kawaida, wachezaji wenzake na klabu angalau wangempa salami za kumtakia heri. Lakini wakati umeshinda taji na siku mbili baadaye una pati kubwa kusherehekea taji na hakuna mtu aliyekwenda kumtakia happy birthday Yaya, nini zaidi unachotaka?
"Ikiwa mchezaji kama Yaya anakwenda Liverpool nawanashinda ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 24, Yaya atakuwa mzuri Liverpool,"alisema Seluk.
Amemtolea mfano beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos alipewa gari aina ya Bugatti Veyron wakati wa birthday yake na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.
Amemtolea mfano beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos alipewa gari aina ya Bugatti Veyron wakati wa birthday yake na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.
Gari iendayo kasi: Mwanasoka mstaafu wa Brazil, Roberto Carlos akiingia kwenye Bugatti Veyron lake
Gari zuri: Seluk amesema Carlos alipewa gari hili na Anzhi Makhachkala katika birthday yake



.png)
0 comments:
Post a Comment