TIMU ya Hispania imefanikiwa kutwaa Kombe la Dunia baada ya kuwafunga waliokuwa mabingwa watetezi, Argentina bao 1-0 usiku huu katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 na ushei Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, Bergen County, New Jersey nchini Marekani.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres García dakika ya 106 akimalizia pasi ya winga wa Athletic Bilbao, Nicholas Williams Arthuer mwenye asili ya Ghana.
Hispania ilicheza pungufu dakika zote 30 za nyongeza baada ya kiungo wake, Enzo Jeremías Fernández anayechezea klabu ya Chelsea ya England kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu beki wa Barcelona na Hispania, Pau Cubarsí Paredes dakika ya 90’+3.
Gwiji wa Argentina alikuwa mnyonge wa kutia huruma baada ya kipyenga cha mwisho akimshuhudia mchezaji aliyempakata akiwa mtoto, Lamine Yamal Nasraoui Ebana wa Barcelona mwenye asili ya Morocco kupitia kwa baba yake na Equatorial Guinea kupitia kwa mama yake akiiongoza La Roja kutwaa Kombe.







.png)
0 comments:
Post a Comment