MABINGWA watetezi, Argentina wamefanikiwa kwenda Fainali ya kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya England usiku huu Uwanja wa Mercedes-Benz Jijini Atlanta Georgia, Marekani.
Hukuwa ushindi mwepesi kwa La Selección baada ya Three Lions kutangulia kupata bao lililofungwa na winga wa Barcelona ya Hispania, Anthony Michael Gordon dakika ya 55 akimalizia krosi ya kiungo mshambuliaji wa Aston Villa ya kwao, England, Morgan Elliot Rogers mwenye asili ya Jamaica kutoka upande wa kulia.
Argentina ikazinduka dakika za mwishoni kama kawaida yake kwenye michuano yam waka huu kwa mabao ya kiungo wa Chelsea ya England, Enzo Jeremías Fernández dakika ya 85 na mshambuliaji wa Inter Milan ya Italia, Lautaro Javier Martínez dakika ya 90’+2, wote wakimalizia pasi za kiungo mshambuliaji wa Inter Miami ya Marekani, Lionel Andrés Messi.
Sasa Argentina watakutana na Hispania katika Fainali ya Kombe la Dunia Julai 19, mwaka 2026 Uwanja wa MetLife Jijini East Rutherford, in Bergen County, New Jersey nchini Marekani.
Kwa upande wao England watawania nafasi ya tatu dhidi ya Ufaransa mchezo utakaotangulia Julai 18 Uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens, Florida, Marekani.
Ikumbukwe Hispania ilitinga Fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa usiku wa jana Uwanja wa AT&T Jijini Arlington, in Tarrant County, Texas nchini Marekani.
Mabao ya La Roja jana yalifungwa na mshambuliaji wa Real Sociedad ya kwao, Hispania, Mikel Oyarzabal Ugarte dakika ya 22 kwa penalti na beki wa kulia wa club Tottenham Hotspur ya England, Pedro Antonio Porro Sauceda dakika ya 58.



.png)
0 comments:
Post a Comment