Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UCHAGUZI mkuu wa Simba SC sasa umepangwa kufanyika Juni 29 mwaka
huu baada ya tarehe iliyokuwa imepangwa awali Mei 3 mwaka huu kupanguliwa baada
ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo na Klabu kukataa kuipitisha Katiba ya
klabu hiyo iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya Simba SC zilizopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam mchana huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damas Ndumbaro amesema kamati yake iliyokutana jijini Dar es Salaam jana, imeamua uchaguzi huo ufanyike Juni 29 kupata Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa kamati mpya ya utendaji ya Simba. "Kamati yangu ina watu makini, waadilifu na wenye mawazo
chanya kwa klabu ya Simba. Mara baada ya msajili kupitisha katiba juzi, jana
tulikutana mara moja kupanga ratiba ya uchaguzi. Hatutakuwa na huruma dhidi ya
watu watakaokiuka kanuni za uchaguzi," amesema Ndumbaro mwenye PhD ya
Sheria.
Kuchelewa kwa uchaguzi huo kunaufanya uongozi
wa sasa chini ya mwenykiti Ismail Aden Rage kuzidisha muda wake wa miaka nminne
tangu Mei 10, 2010 unaolizika Mei 10 mwaka huu, Jumamosi ijayo.
RATIBA YA MCHAKATO UCHAGUZI SIMBA SC
Mei 9, 2014: Kwanzaa kutoa fomu
Mei 14, 2014: Kurudisha fomu
Mei 17, 2014: Uhakiki wa fomu za wagombea
Mei 19, 2014: Kutangaza majina ya wagombea
Mei 20, 2014: Kupokea pingamizi dhidi ya wagombea
Mei 25, 2014: Kusikiliza pingamizi
Mei 27, 2014: Usaili wa wagombea
Mei 29, 2014: Kutangaza matokeo ya usaili
Mei 30, 2014: Masula ya kimaadili
Juni 2-9, 2014: Kukata rufaa kamati ya rufaa
Juni 2-7, 2014: Maamuzi ya kamati ya maadili
Juni 10-12, 2014: Kusikiliza rufaa Juni 8-12
Juni 16, 2014: Kukata rufaa kamati ya rufaa ya maadili
Juni 16-20, 2014: Maamuzi ya mwisho ya kamati ya rufaa na kamati ya rufaa ya maadili
Juni 21-23, 2014: Kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
Juni 24-28, 2014: Kampeni
Juni 29, 2014: Uchaguzi mkuu

0 comments:
Post a Comment