// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMIR NASRI AZIDI KUWAZIBA MIDOMO WABAYA WAKE MAN CITY IKIUA 3-0 UARABUNI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMIR NASRI AZIDI KUWAZIBA MIDOMO WABAYA WAKE MAN CITY IKIUA 3-0 UARABUNI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 15, 2014

    SAMIR NASRI AZIDI KUWAZIBA MIDOMO WABAYA WAKE MAN CITY IKIUA 3-0 UARABUNI

    KIUNGO Samir Nasri ameendeleza wiki nzuri za mafanikio katika soka, baada ya jioni ya leo kufanya kazi nzuri Manchester City ikicheza mchezo wa kirafiki na Al Ain katika ziara yake ya Falme za Kiarabu. 
    Mfaransa huyo atakwenda na kulala na tabasamu zuri baada ya kutengeneza mabao mawili katika ushindi wa 3-0 wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Hazza bin Zayed.

    Anakwenda na mpira: Nyota wa Manchester City, Samir Nasri akimtoka beki wa Al Ain katika mchezo wa kirafiki leo
    Greeting: At least this fan was happy to see Manchester City forward Samir Nasri
    Greeting: At least this fan was happy to see Manchester City forward Samir Nasri
    Tunakupenda: Shabiki huyo alishindwa kujizuia na kuvamia uwanjani kwenda kumbusu Samir Nasri

    Akiwa na machungu ya kutemwa na kocha Didier Deschamps katika kikosi cha Ufaransa cha Kombe la Dunia, Nasri alipambana kuhakikisha anawaziba midomo wanaomkandia baada ya demu wake, kutweet matusi dhidi ya timu ya taifa.
    Ameacha miguu yake izungumze, akiwapasia mipira ya kufunga Marco Lopes dakika ya 63 na Stevan Jovetic dakika ya 78 katika me chi ambayo wenyeji walibadilisha wachezaji 25. 
    Bao lingine la City lilifungwa na Hiwula kwa penalti dakika ya 89 katika mechi iliyohudhuriwa na watu 21,437. Al Ain ndiyo klabu yenye mafanikio zaidi kihistoria UAE na Jumapili itacheza Fainali ya Kombe la Rais. Delight: Marcos Lopes celebrates after scoring the opening goal for Manchester City against Al Ain
    Marcos Lopes akishangilia bao lake dhidi ya Al Ain
    Worthy of applause: Manchester City owner Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan cheers his team on from inside the Hazza bin Zayed Stadium
    Mwenye timu: Mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan akipiga makofi Uwanja wa Hazza bin Zayed leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMIR NASRI AZIDI KUWAZIBA MIDOMO WABAYA WAKE MAN CITY IKIUA 3-0 UARABUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top