• HABARI MPYA

    Saturday, July 18, 2026

    AZAM FC YASAJILI BEKI MWINGINE MKONGO

     KLABU ya Azam FC imemtambulisha winga, Henoc Molia (22) kutoka St. Eloi Lupopo ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mchezaji wake mpya wa nne kuelekea msimu ujao.

    Wengine ni mabeki wa kati, Lupini Mawuku Dieumerci (20) kutoka AS Maniema Union ya kwao, DRC na Henri Braham Stanic Mbelgiji mwenye asili ya DRC pia kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, wakati mchezaji mwingine ni winga Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon ‘Kipre Junior’ aliyejiunga tena na Azam FC akitokea MC Algiers ya Algeria. 

    Kipre Junior amerejea Azam FC ambako awali alicheza kuanzia msimu wa 2022-2023 akitokea SOL FC d’Abobo ya kwao, Ivory Coast hadi 2024-2025 alipohamia MC Algiers.


    @azamfcofficial

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI BEKI MWINGINE MKONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top