• HABARI MPYA

    Sunday, July 12, 2026

    ARGENTINA YAIFUATA ENGLAND NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Argentina imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uswisi katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 Alfajiri ya leo Uwanja wa Arrowhead, Kansas City, Missouri, Marekani. 
    Mabao ya Argentina yamefungwa na kiungo wa Liverpool ya England, Alexis Mac Allister dakika ya 10 na washambuliaji, Julián Alvarez wa Atlético Madrid ya Hispania dakika ya 112 na Lautaro Javier Martínez wa Inter Milan ya Italia dakika 120.
    Kwa upande wao Uswis bao Lao pekee limefungwa na winga wa Nottingham Forests ya England, Dan Assane Ndoye mwenye asili ya Senegal dakika ya 67.
    Argentina sasa itakutana na England katika mechi kali ya Nusu Fainali Julai 15 Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia nchini Marekani.
    England ilitangulia Nusu baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Norway usiku wa kuamkia  leo Uwanja wa Hard Rock Jijini Miami Gardens, Dade County, Florida, Marekani.
    Mabao yote ya Three Lions yalifumgwa na kiungo mshambuliaji Jude Victor William Bellingham mwenye asili ya Kenya anayechezea klabu ya Real Madrid ya Hispania aliyefunga dakika ya  45’+2 na 93 katika mchezo uliodumu kwa dakika 120.
    Kwa upande wao Norway bao lao pekee amefunga kiungo mshambuliaji wa Benfica ya Ureno,  Andreas Rædergård Schjelderup dakika ya 36.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARGENTINA YAIFUATA ENGLAND NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top