• HABARI MPYA

    Monday, July 09, 2012

    AZAM, SIMBA KAZINI ZANZIBAR LEO


    MASHINE; Sunzu, ataibeba simba na leo?

    Na Prince Akbar,
    MICHUANO ya Kombe la Urafiki visiwani Zanzibar, leo inafikia hatua ya Nusu Fainali kwa mechi mbili kupigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watacheza na Zanzibar All Stars kuanzia saa 2:00 usiku, wakati Azam FC watamenyana na Super Falcon kuanzia saa 10:30 jioni.
    Azam na Simba, zote zimefuzu kutoka Kundi A wakati All Stars na Falcon zimetokea Kundi B, lililokuwa na Yanga pia, ambayo iliondolewa kwa kupeleka watoto.
    Simba SC ni mabingwa wa Bara, Falcon ni mabingwa wa Zanzibar, Azam FC ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi na washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara wakati Falcon inaundwa na mseto wa wachezaji nyota wa Zanzibar.
    Katika mechi yake ya mwisho ya Kundi A, Simba iliifunga kwa taabu Karume Boys 1-0, bao pekee la mshambuliaji wake Mzambia, Felix Mumba Sunzu Jr, wakati Azam iliifunga Mafunzo 3-2.
    ADEBAYOR WA CHAMAZI; Ataibeba Azam leo?
    Kuna uwezekano mkubwa Simba na Azam zikakutana katika Fainali Jumatano, kwani zinapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi zao leo, ingawa pia haitarajiwi kuwa kazi nyepesi kwani timu za Zanzibar nazo zimeimarika siku za karibuni.
    Katika mchezo wa leo, huanda kocha wa Simba Profesa Milovan Cirkovick akapanga kikosi hiki; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba/Edward Chirtopher, Mwinyi Kazimoto/Salim Kinje, Mussa Mudde/Jonas Mkude, Felix Sunzu/Abdallah Juma, Kanu Mbivayanga/ Uhuru Suleiman na Danny Mrwanda/Abdallah Seseme.
    Kwa upande wa Azam, inawezekana Stewart Hall, akawapanga: Deo Munishi ‘Dida’, Samir Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Said Mourad, Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Kipre Herman Tcheche, Kipre Michael Balou, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Gaudence Mwaikimba na George Odhiambo ‘Blackberry’/Hamisi Mcha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM, SIMBA KAZINI ZANZIBAR LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top