• HABARI MPYA

    Thursday, July 12, 2012

    AZAM ACADEMY WACHEZA MBELE YA RAIS BURUNDI LEO

    TIMU ya soka ya vijana ya Azam FC, maarufu kama Azam Academy leo inacheza mechi ya kukamilisha ratiba kwenye michuano ya Rollingston inayoendelea nchini Burundi, katika mechi ambayo mgeni rasmi atakuwa rais wa Burundi, Perre Nkurunziza.
    Azam tayari imekwishafuzu Robo Fainali, baada ya kushinda mechi zake mbili za awali 1-0 dhidi ya Kyazanga FC ya Uganda na 3-0 dhidi ya Nyirakongo Academy ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Katika mchezo huo, kikosi cha Azam kinatarajiwa kuwa; Aishi, Mgaya, Shabalala, Dizana, Mkomola, Reyna, Mudathiri, Kaijage, Machuppa, Kelvin na Kimwaga.
    Simba na Yanga zilialikwa pia kwenye michuano hiyo, ila zote zimejitoa dakika za mwishoni.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM ACADEMY WACHEZA MBELE YA RAIS BURUNDI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top