• HABARI MPYA

    Friday, July 10, 2026

    UFARANSA YAICHAPA MOROCCO 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Ufaransa imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa Robo Fainali usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Gillette Jijini Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani. 
    Mabao yote ya Ufaransa yamefungwa na washambuliaji wake wenye asili ya Afrika, Kylian Mbappé Lottin wa Real Madrid ya Hispania mwenye asili ya Cameroon dakika ya 60 na Masour Ousmane Dembélé wa  Paris Saint-Germain ya Kwai, Paris mwenye asili ya Mauritania, Senegal na Mali dakika ya 66.
    Ufaransa wanders kuondoka na ushindi mnene zaidi kama Nahodha wake, Mbappe asingekosa penalti dakika ya  28, ambayo iliokolewa na kipa wa Al Hilal ya Saudi Arabia, Yassine Bounou mzaliwa wa Canada.
    Sasa Ufaransa itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya pili kati ya Hispania na Ubelgiji zitakazomenyana leo Uwanja wa SoFi, Inglewood, Kusini-Magharibi mwa Los Angeles, California, Marekani.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UFARANSA YAICHAPA MOROCCO 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top