• HABARI MPYA

    Saturday, July 11, 2026

    HISPANIA YAICHAPA UBELGIJI 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Hispania imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji usiku huu Uwanja wa SoFi Jijini Inglewood, Los Angeles, California, Marekani.
    Mabao ya La Roja yamefungwa na kiungo wa Paris Saint-Germain ya Ufaransa, Fabián Ruiz Pena dakika ya 30 na mshambuliaji wa Arsenal ya England, Mikel Merino Zazón dakika ya 88, wakati bao pekee la 'Mashetani Wekundu’ limefungwa na mshambuliaji wa Atalanta ya Italia, Charles Marc S. De Ketelaere dakika ya 41.
    Dalili za jahazi la Ubelgiji kuzama leo zilionekana pale kipa wake wa kwanza, Thibaut Courtois wa Real Madrid ya Hispania alipoumia paja na kulazimika kutoka dakika ya 71 nafasi yake ikichukuliwa na kipa wa akiba wa Manchester United ya England, Senne Lammens aliyedaka mechi yake ya kwanza timu yake hiyo ya taifa.
    Kwa ushindi huo, Hispania watakutana na Ufaransa katika Nusu Fainali kali kabisa Julai 14 Uwanja wa AT&T Jijini Arlington, Tarrant County, Texas, hapo hapo Marekani.

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HISPANIA YAICHAPA UBELGIJI 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top