• HABARI MPYA

    Tuesday, June 16, 2026

    UBELGIJI YAAMBULIA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA MISRI KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Ubelgiji imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Misri katika mchezo wa Kundi G Fainali za Kombe la Dunia usiku huu Uwanja wa Lumen Field Jijini Seattle, Washington, Marekani.
    Kiungo Emam Ashour Metwally Abdel Ghany alianza kuifungia Misri dakika ya 19, kabla ya mchezaji mwenzake wa Al Ahly ya nyumbani, Cairo – beki Mohamed Hany Gamal El-Demerdash kujifunga dakika ya 66 katika jitihada za kuokoa na kujiikuta anaipatia Ubelgiji bao la kusawazisha.
    Mchezo mwingine wa Kundi G utafuatia baadaye kati ya Iran na New Zealand Uwanja wa SoFi Jijini Inglewood, Los Angeles, California, Marekani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UBELGIJI YAAMBULIA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA MISRI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top