• HABARI MPYA

    Saturday, September 01, 2018

    MTIBWA SUGAR, TANZANIA PRISONS, STAND UNITED ZATEMBEZA VICHAPO LIGI KUU…COASTAL UNION WABANWA NYUMBANI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Mtibwa Sugar imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi za nyumbani za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuichapa Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
    Ushindi huo umetokana na mabao ya mshambuliaji Stahmili Mbonde dakika ya tisa na kiungo Ismail Muhesa dakika ya 42, wakati bao pekee la Mbeya City limefungwa na Erick Kyaruzi dakika ya 48.
    Huo ni ushindi wa pili mfululizo dhidi ya timu za Mbeya baada ya kuifunga Tanzania Prisons 1-0 Agosti 26 mjini Morogoro wakitoka kufungwa 2-1 na Yanga Agosti 23 kwenye mchezo wa kwanza wa msimu.

    Mshambuliaji Stahmili Mbonde (kushoto) akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Mtibwa Sugar dakika ya tisa

    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabao ya Laurian Mpalile dakika ya 20 na Ramadhani Ibata dakika ya 85.
    Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, bao pekee la mshambuliaji Mrundi, Bigirimana Blaise dakika ya 61 limetosha kuipa pointi tatu Stand United baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United ya Mara.
    Coastal Union imalazimishwa sare ya 1-1 na KMC ya Dar es Salaam Uwanja wa Mkwakwani huko Tanga, wenyeji wakitangulia kwa bao la Hamisi Kanduru dakika ya 33 kabla ya Cliff Buyoya kuisawazishia timu ya Manispaa ya Kinondoni dakika ya 79 na Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na African Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR, TANZANIA PRISONS, STAND UNITED ZATEMBEZA VICHAPO LIGI KUU…COASTAL UNION WABANWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top