• HABARI MPYA

    Thursday, September 27, 2018

    UJERUMANI WENYEJI WA EURO 2024, UTURUKI CHALI UEFA

    UJERUMANI imeshinda haki ya kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024, ikiwazidi Uturuki katika kura zilizopigwa na Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) mjini Nyon, Uswisi.
    Washindi mara tatu wa mashindano hayo, Ujerumani walikuwa wenyeji wa fainali za mwaka 1988 na pia wamewahi kuandaa Fainali za Kombe la Dunia katika miaka ya 1974 na 2006.
    Pia watakuwa wenyeji wa michuano ya Olimpiki katika Jiji la Berlin itakayoshirikisha timu 24, na jumla ya michezo 51 kwa siku 32 kati ya Juni na Julai. 

    Ujerumani ndiyo wenyeji wa Euro 2024 baada ya kuwazidi Uturuki 



    MICHUANO YA SOKA YA KIMATAIFA  

    Euro 2020 (Ulaya pekee)

    Kombe la Dunia 2022 (Qatar)

    Euro 2024 (Ujerumani)

    Kombe la Dunia 2026 (Amerika Kaskazini) 
    Miji mingine itakayotumika kwa Michezo hiyo ni Cologne, Dortmund, Dusseldorf, Frankfurt, Gelsenkirchen, Hamburg, Leipzig, Munich na Stuttgart.
    Hii ni mara ya tano Uturuki wanashindwa katika jitihada zao za kuutaka yenyeji wa Euro na walitarajiwa sana kupata uenyeji wa sherehe za kutimiza miaka 100 kwa fainali za 2024  ambazo zingekuwa za kwanza kubwa za soka kuandaa.
    Wakati Ujerumani ilibebwa na viwanja vyake vizuri, hoteli bora na usafiri na miundombinu, Uturuki iliangushwa na Viwanja vyake vya Ndege, Reli, Barabara na Viwanja pia kuwa katika ubora usioridhisha na pia hali ya kiuchumi ya nchi yake kwa sasa kuwa mbaya.
    Lakini pia na nchi hiyo kuwa na rekodi mbaya ya haki za binadamu iliyopatikana katika taarifa ya thamini za UEFA, nayo imewaangusha.
    Rais wa Shirikisho la Soka la Ujerumani, Reinhard Grindel na Makamu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Uturuki, Servet Yardimci hawakuruhusiwa kupiga kura na wa Denmark pia, Lars-Christer Olsson, uamuzi huo ulichukuliwa kwa kura za Wajumbe wengine 17 wa Kamati Kuu ya UEFA.
    Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo, Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin alisema: "Kulikuwa kuna wagombe wawili wa nguvu kutoka nchi kubwa kisoka, lakini bahati mbaya lazima mmoja ashinde,".
    "Utaratibu ulikuwa wazi na kura zilikuwa za kidemkrasia na ninaamini maamuzi yoyote ya Kidemokrasia ni ya haki. Nachoweza kusema ni tu sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye michuano ya Euro ya 2024," amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UJERUMANI WENYEJI WA EURO 2024, UTURUKI CHALI UEFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top