• HABARI MPYA

  Tuesday, September 25, 2018

  NI LUKA MODRIC MWANASOKA BORA WA DUNIA WA FIFA 2018

  Luka Modric amemaliza utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika tuzo za Wachezaji Bora binafsi duniani.

  WASHINDI WOTE WA TUZO ZA FIFA 2018: 

  Tuzo ya Puskas
  Mohamed Salah
  Kocha Bora wa Kiume wa Mwaka 
  Didier Deschamps
  Kocha Bora Kike wa Mwaka
  Reynald Pedros 
  Kipa Bora wa Mwaka
  Thibaut Courtois 
  Mwanasoka Bora wa Kike 
  Marta
  Tuzo ya Mwanasoka  Bora wa Kiume wa Mwaka wa FIFA
  Luka Modric
  Kikis Bora cha FIFA FIFPro
  David De Gea; Dani Alves, Raphael Varane, Sergio Ramos, Marcelo; Luka Modric, N'Golo Kante, Eden Hazard; Lionel Messi, Kylian Mbappe, Cristiano Ronaldo.
  KIUNGO Luka Modric amemaliza zama za utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika tuzo za Wachezaji Bora binafsi duniani.
  Hiyo ni baada ya Modric kuwazidi wapinzani wake, Ronaldo na Mohamed Salah wa Liverpool na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa Mwaka wa FIFA katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Royal Festival mjini London.
  Na hiyo ni baada ya Modric kufanya vizuri katika klabu yake, Real Madrid mwaka 2018 akiiwezesha kushinda mataji ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kuiongoza timu yake ya taifa, Croatia kufika fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi ambako ilifungwa na Ufaransa. 
  "Ni heshima kubwa na hisia nzuri kusimama hapa na taji hii maridadi," Modric said.
  "Kwanza kabisa ningependa kuwapongeza Mohamed na Cristiano kwa msimu mzuri waliokuwa nao.
  "Taji hili si la kwangu tu, ni la wachezaji wenzangu pia wa Real Madrid, la wachezaji wenzangu wote wa timu ya taifa ya Croatia, ya makocha wote niliocheza timu zao. Bila wao, hili lisingewezakana,". 
  Kisha Modric akamgeukia kiungo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Misri, Salah, aliyehudhuria tuzo hizo huku nyota mkubwa wa Juventus, Ronaldo akibaki Italia.
  "Nina uhakika siku zijazo utapata nafasi nyingine ya kupigania tuzo hii,"alimalizia.
  Mchezaji mwenzake Modric, Gareth Bale amempogeza kwa ushindi huyo kupitia akaunti yake ya Instagram:?
  Nyota wa zamani, Mbrazil Brazil Pele pia amempongeza Modric kwa ushindi huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI LUKA MODRIC MWANASOKA BORA WA DUNIA WA FIFA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top