• HABARI MPYA

  Monday, September 24, 2018

  SAMATTA ATOA PASI YA BAO KRC GENK YASHINDA 5-2 UGENINI LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, BRUGGE 
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu amecheza kwa dakika 85 na kutoa pasi ya bao moja, timu yake, KRC Genk ikipata ushindi wa mabao 5-2 ugenini kwa Cercle Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge, Samatta alitoa pasi ya bao la nne lililofungwa na mshambuliaji wa kinda wa umri wa miaka 23, Mbelgiji Leandro Trossard ambaye alifunga mabao matatu peke yake.

  Mbwana Samatta akimpongeza Leandro Trossard baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa 5-2 

  Trossard alifunga mabao yake katika dakika za 43, 78 na 82 wakati mabao mengine ya Genk yamefungwa na Joakim Mæhle dakika ya kwanza na Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 54.
  Mshambuliaji Mbelgiji Gianni Bruno akamsetia Guevin Tormin kuifungia kwa Cercle Brugge bao la kwanza dakika ya 32, kabla yay eye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 56.
  Kikosi cha Cercle Bruges kilikuwa; Nardi, Palun, Ueda, Lambot, Etienne, Kone/Bongiovanni dk66, Lusamba, Omolo/Gakpe dk56, Mercier, Tormin na Bruno/De Belder dk75.
  KRC Genk: Vukovic, Maehle, Aidoo, Lucumi, Uronen, Berge, Pozuelo, Malinovskyi/Heynen dk45, Paintsil/Ndongala dk62, Trossard na Samatta/Gano dk85.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOA PASI YA BAO KRC GENK YASHINDA 5-2 UGENINI LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top