• HABARI MPYA

    Friday, September 21, 2018

    ESPERANCE YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

    TIMU ya Esperance ya Tunisia imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Etoile du Sahel, zote za Tunisia usiku wa Jumamosi Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse.
    Bao pekee la Esperance katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Muivory Coast, Fousseny Coulibaly dakika ya 87 akimalizia pasi ya beki mkongwe wa umri wa miaka 31, Mtunisia, Sameh Derbali.
    Ushindi huo wa ugenini katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali unaifanya Esperance isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya awali kushinda 2-1 Jumamosi kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Olimpiki wa Rade.

    Mchezo mwingine wa Robo Fainali leo, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetupwa nje kwa mabao ya ugenini, baada ya Mazembe kulazimishwa sare ya 1-1 na C.D. Primeiro de Agosto Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.
    Mshambuliaji kinda wa miaka 20 wa DRC, Jackson Muleka aliifungia bao la kuongoza Mazembe mapema tu dakika ya 12, akimalizia pasi ya kiungo Muivory Coast, Christian Raoul Kouame Koffi.
    Lakini TP Mazembe ikashindwa kujilinda na kuwaruhusu wageni kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji Mkongo pia, Mongo Kipe Lumpala Bokamba dakika ya 34 akimalizia pasi ya mshambuliaji Muangola, Hermenegildo Costa Paulo Bartolomeu.
    Na kwa sababu mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 0-0 Jumamosi Uwanja wa Estádio 11 de Novembro mjini Luanda, Primeiro de Agosto inakwenda Nusu Fainali kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 1-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ESPERANCE YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top