• HABARI MPYA

  Wednesday, September 26, 2018

  SINGIDA UNITED WAZINDUKA, WAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 NAMFUA KIPA MMALAWI AFUNGWA BAO AIBU TUPU

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Namfua mjini Singida.
  Mshambuliaji mpya, Habib Hajji Kiyombo aliyesajiliwa kutoka Mbao FC ya Mwanza aliifungia Singida bao la kwanza kwa penalti dakika ya 24, kufuatia Nahodha wa Mbeya City, Erick Kyaruzi kuunawa mpira wa adhabu uliopigwa na John Tibar George.
  Tibar mwenyewe akaifungia bao la pili Singida United dakika ya 67 baada ya kuunasa mpira uliopigwa na mchezaji wa Mbeya City na kuingia nao ndani kidogo ya boksi kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Mmalawi, Owen Chaima.


  Chaima akawazawadia bao la tatu rahisi kabisa Singida baada ya shuti lililoonekana halina madhara la Yusuph Kagoma kumpita dakika ya 89. 
  Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ ifikishe pointi 10 baada ya kucheza mechi saba, ikishinda tatu, sare moja na kufungwa nne.
  Kwa MCC baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi zake saba za mechi saba, ikiendeleza rekodi ya kufanya vibaya katika mechi zote za ugenini. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WAZINDUKA, WAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 NAMFUA KIPA MMALAWI AFUNGWA BAO AIBU TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top