• HABARI MPYA

  Monday, September 24, 2018

  ENYIMBA YAITUPA NJE RAYON KOMBE LA SHIRIKISHO, YAIPIGA 5-1

  TIMU ya Enyimba International imeitupa nje Rayon Sport ya Rwanda katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuichapa mabao 5-1 katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Enyimba International mjini Aba, Nigeria. 
  Enyimba inakwenda Nusu Fainali kibabe baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na Rayon Sport kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda wiki iliyopita.
  Katika mchezo wa jana, mabao ya Enyimba yalifungwa na Stanley Dimgba dakika ya 12, Ikouwem Utin dakika ya 29, Sunday Adetunji dakika ya 48, Joseph Osadiaye dakika ya 60 na Isiaka Oladuntoye dakika ya 80, wakati la Rayon lilifungwa na Bonfilscaleb Bimenyimana dakika ya 24. 

  Mechi nyingine za marudiano za Robo Fainali jana, bao pekee la mshambuliaji mkongwe wa umri wa miaka 33, Mouhssine Lajour dakika ya nne liliipa ushindi wa 1-0 Raja Casablanca dhidi ya CARA Brazzaville Uwanja wa Mfalme Mohamed V mjini Casablanca.
  Raja inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1, kufuatia kushinda 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Septemba 16 Uwanja wa Alphonse Massamba-Debat mjini Brazzaville.
  Al Masry ya Misri ikapata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, USM Alger bao pekee la Mahmoud Wadi dakika ya 34 akimalizia pasi ya Mohamed GrendoUwanja wa Mei 8 Mai, 1945 mjini Setif na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.
  RSB Berkane ikalazimishwa sare ya 1-1 na Vita Club Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane, Algeria nchini Morocco na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kufungwa 3-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Kinshasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENYIMBA YAITUPA NJE RAYON KOMBE LA SHIRIKISHO, YAIPIGA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top