• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2018

  WEZI WAVAMIA MAKAO MAKUU YA KLABU YA LIPULI FC IRINGA, WAVUNJA NA KUIBA JEZI ZOTE ZA TIMU

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  OFISI za klabu ya Lipuli FC mjini Iringa zimevamiwa na watu wasiojulikana ambao wameiba jezi zote za timu hiyo zilizotengwa maalum kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC).
  Taarifa ya Lipuli FC kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba wezi hao walifanikiwa kuingia kwenye ofisi za klabu baada ya kuvunja kufuli la mlango wa ofisi kwa kutumia nondo.
  “Kumetokea tukio la wizi katika ofisini zetu za klabu ya Lipuli Fc usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kuiba jezi zote za FA CUP pamoja na mavazi ya kusafiria. Wezi hao wamevunja kufuli la mlango wa ofisi kwa kutumia nondo,” imesema taarifa hiyo.

  Uongozi wa Lipuli umesema kwamba Sekretarieti ya klabu imechukua hatua muhimu ya kuripoti tukio hilo kwa vyombo vya usalama, kwa maana ya jeshi la Polisi na kupewa taarifa ya tukio, ijulikanayo kama  RB namba 6605/20/8.
  Wezi hao walitumia mwanya wa uongozi wa klabu kuwa na timu mjini Dar es Salaam ambako juzi walicheza mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania na kupata sare ya 0-0 na wenyeji, Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEZI WAVAMIA MAKAO MAKUU YA KLABU YA LIPULI FC IRINGA, WAVUNJA NA KUIBA JEZI ZOTE ZA TIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top