• HABARI MPYA

  Friday, September 21, 2018

  MAKOCHA WOTE WASAIDIZI WAACHIA NGAZI SINGIDA UNITED SABABU YA MALIPO YAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAKOCHA wote Wasaidizi wa Singida United, Jumanne Challe na Mfaume Athumani, kocha wa makipa wamejitoa kwenye timu hiyo wakishinikiza kulipwa stahiki zao.
  Wawili hao hawakuwepo benchi jana wakati Singida United ikichapwa mabao 3-2 na wenyeji, African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam japokuwa walisafiri na timu kutoka Singida.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online baada ya kuulizwa juu ya kutokuwepo benchi jana, Samatta, kipa wa zamani wa Yanga SC alisema kwamba wamejiondoa kwa sababu hawana mikataba na pia wanadai fedha zai nyingi.
  Mfaume Athumani na Jumanne Challe wamejiondoa Singida United 

  “Nimekuja Dar es Salaam, lakini mimi nina madai yangu hawajanipa bado na sina mkataba nao. Siwezi kuendelea kufanya kazi bila mkataba,”amesema baada ya kuulizwa juu ya kutokuwepo benchi jana.
  Samatta ambaye amekuwa kocha wa makipa wa Singida United tangu msimu uliopita timu ilipopanda, ameongeza kwamba amekuwa aifuatilia suala la mkataba na haki zake, lakini kwa msimu wa pili sasa utekelezaji umekuwa tatizo.
  “Tangu timu ianze Ligi Kuu nimekuwa ninafanya kazi bila mkataba, nilikuwa ninafanya kazi kama kibaruwa na kila nikiomba mkataba wananizungusha. Na tumeondoka na Challe pia, tunadai fedha nyingi hatujalipwa. Kama wanataka turudi kazini watupe stahiki zetu,”amesema.
  Kwa upande wake, Samatta amesema tayari ana ofa kutoka timu tatu ambazo atajiunga nazo iwapo Singida itashindwa kumlipa haki zake arejee kazini. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKOCHA WOTE WASAIDIZI WAACHIA NGAZI SINGIDA UNITED SABABU YA MALIPO YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top