• HABARI MPYA

    Saturday, September 01, 2018

    KARIA AAHIDI KUWAPATIA MECHI KUBWA ZA KIMATAIFA TWIGA STARS WAKUZE UWEZO WATISHE ZAIDI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameahidi kuitafutia mechi ngumu timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars dhidi ya timu za mataifa makubwa kisoka ili kuijengea uwezo zaidi.
    Karia ametoa ahadi leo mjini Dar es Salaam alipokuwa akitoa pongezi zake kwa Twiga Stars baada ya kutwaa Kombe la Ubingwa wa Jumuiya ya Africa Mashariki nchini Burundi wiki iliyopita.
    "Shirikisho litafanya mpango wa kutafuta mechi za kirafiki na mataifa yenye ushindani ili kuimarisha kikosi chenu cha Twiga Stars," amesema.

    Shabiki huyo wa Coastak Union ya Tanga, amesema kwamba mechi hizo zitakuwa dhidi ya mataifa ambayo yamekuwa kikwazo kwa Tanzania.
    Pamoja na pongezi hizo, Karia amewataka wachezaji wa Twiga Stars kudumisha nidhamu kuanzia kwenye klabu zao, kwani huo ndio msingi wa mafanikio ambayo yanapatikana kwenye mashindano mbalimbali.
    Amewataka kwenda na nidhamu hiyo mpaka kwenye ngazi ya klabu ambako wanarudi sasa baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa na waepukane na tabia hatarishi.
    “Mafanikio mnayoyapata msingi wake ni nidhamu mliyonayo nashukuru sijawahi kusikia nidhamu mbaya katika timu hii,ni vyema pia mkajiepusha na tabia hatarishi” alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.
    Wachezaji wa kikosi cha Twiga Stars wameruhusiwa kurudi kwenye timu zao mpaka hapo watakapoitwa kwa maandalizi ya mechi mbalimbali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KARIA AAHIDI KUWAPATIA MECHI KUBWA ZA KIMATAIFA TWIGA STARS WAKUZE UWEZO WATISHE ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top