KLABU ya Simba SC imemtambulisha winga wa kushoto wa Kimataifa wa Senegal, Libasse Gueye (22) kuwa mchezaji wake mpya akijiunga na Wekundu hao Msimbazi kutoka Teungueth FC ya kwao.
Libasse Gueye aliibukia kwenye kituo cha vijana cha Demba Diop ambako alicheza hadi timu ya chini ya umri wa miaka 20 (Demba Diop U20) kabla ya kujiunga na klabu ya Diambars FC ya League 1 Senegal.
Januari mwaka 2022 alipelekwa kwa mkopo Valencia U19 hadi Juni 30 akarejea Diambars FC ambayo Agosti mwaka huo ilimuuza Pontevedra CF ya Daraja la Tatu Hispania ambako alicheza hadi Julai 2024 aliporejea Senegal na kukaa bila timu hadi aliposajiliwa na Teungueth FC Desemba 3 mwaka juzi.



.png)
0 comments:
Post a Comment