• HABARI MPYA

  Sunday, September 23, 2018

  KINYOZI WA MBAGALA AJISHINDIA BAJAJI YA SPORTPESA PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI

  PROMOSHENI ya shinda zaidi na SportPesa imeanza kwa kasi na safari hii mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam amejishindia Bajaj mpya baada ya kubashiri na SportPesa.
  Abdallah Selemani Ally (29), ambaye ni kinyozi amekuwa mshindi wa pili wa Bajaj mpya kutoka SportPesa baada ya kubashiri na kuingia kwenye droo iliyochezeshwa kwenye ofisi za kampuni hiyo.  
  Akiongea mara baada ya ushindi huo, Ally amesema alikuwa na ndoto ya kushinda Bajaj tangu promosheni iliyopita.  
  "Nimefurahi sana kushinda na SportPesa nilianza kucheza na SportPesa miezi tisa iliyopita na tangu Promosheni Ya Mwanzo ya Bajaji nilipambana kakini Sikushinda" alisema Ally.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas (kushoto) akizungumza  

  “Ila kweli kutokata tamaa kuna faida kwa sababu sikutegemea kabisa kama ningeshinda mwanzoni kwenye promosheni hii" aliongeza Ally.  Promosheni ya shinda zaidi na SportPesa itaendelea kwa siku mia moja ambapo watu wanaobashiri na SportPesa wataingia moja kwa moja kwenye droo kila siku. 
  Hii ni mara ya pili kwa kampuni ya SportPesa kuendesha promosheni inayotoa nafasi kwa watu wote wanaobashiri na kampuni hiyo kushinda Bajaji, akizungumzia hili Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Tarimba Abbas alisema “huyu ni mshindi wetu wa kwanza kutoka Dar es Salaam, mwaka jana Mkoa huu uliongoza kwa kupata washindi zaidi ya 33 ambao walipatikana kutoka kona mbalimbali jijini.
  Natoa rai kwa watanzania wote walioko nchini kushiriki vilivyo ili kuondoka na bajaji mpya kutoka SportPesa na kujikwamua kiuchumi”
  Watu wanaobashiri na SportPesa hawahitaji kufanya chochote zaidi ya kubashiri na namba zao zinaingia moja kwa moja kwenye droo
  SportPesa hivi sasa imewarahisishia wateja wake kwa kuwaboreshea menu ya *150*87# ambayo imekusanya kila kitu kama vile kuweka beti, kupata orodha ya mechi, kuweka fedha, kuangalia beti yako inavyoendelea hivyo kila kitu mteja anaweza maliza hapo Au akacheza kupitia www.Sportpesa.co.tz na kila unapotupia bashiri yako moja Kwa moja umeingia kwenye Droo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KINYOZI WA MBAGALA AJISHINDIA BAJAJI YA SPORTPESA PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top