• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2018

  KATWILA ASEMA MTIBWA SUGAR HAWADHARAU MECHI KWA SABABU LIGI KUU MSIMU HUU NGUMU

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kwamba wao hawadharau mechi kwa sababu Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ni ngumu na hatabiriki, unaweza kushinda au kufungwa popote.
  Akizungumza jana na Manungu, Turiani mkoani Morogoro kuelekea kesho dhidi ya Biashara United ya Mara, Katwila amesema kwamba wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
  Amesema hawawezi kuidharau Biashara United kwa sababu tu imepanda Ligi Kuu msimu huu, kwani nayo ina kikosi kizuri.
  “Ligi ya msimu huu haitabiriki, unaweza kupoteza mechi popote na unaweza kushinda popote, haijalishi iwe nyumbani au ugenini, kwa sababu ligi ni ya ushindani sana, kikubwa ni maandalizi mazuri,”amesema.

  Zuberi Katwila amesema hawadharau mechi kwa sababu Ligi Kuu msimu huu ni ngumu

  Aidha, Katwila amesema kwamba kuelekea mechi ya kesho vijana wake vizuri kabisa na matarajio ni kuendeleza wimbi la ushindi kesho Manungu.
  Amesema kwamba anafurahi wachezaji wako nao wana dhamira ya kushinda mechi zote zijazo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
  Mtibwa Sugar kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 13 baada ya kucheza mechi saba, ikiwa nyuma ya vinara, Mbao FC wenye pointi 13 za mechi saba pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KATWILA ASEMA MTIBWA SUGAR HAWADHARAU MECHI KWA SABABU LIGI KUU MSIMU HUU NGUMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top