• HABARI MPYA

  Saturday, September 22, 2018

  NAHODHA WA STAND UNITED AWAAMBIA NDANDA FC; “TUMEWASOMA, JIPANGENI TUNAKUJA KWA HASIRA”

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Stand United ‘Chama la Wana’, Jackob Massawe amesema kufuatia kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Yanga na KMC wameamua kuelekeza nguvu na akili yao katika mchezo wao na Ndanda FC utakaochezwa Jumatatu mjini Mtwara.
  Akizumzungumza na Bin Zubeiry Sports – Online, Massawe amesema kwamba watautumia mchezo huo kama sehemu ya kusahihisha makosa yao waliyoyafanya katika michezo miwili iliyopita ambapo waliambulia alama sifuri licha ya kuweza kufunga magoli matatu.
  “Tumejipanga kupata ushindi dhidi ya Ndanda, tutatumia makosa tuliyofanya katiki hizi mechi mbili kama sehemu ya darasa letu ili tufanye vizuri, tumewasoma Ndanda katika mchezo wao na Simba tukaona madhaifu yao tutayatumia hayo kujipatia ushindi,”alisema Jacob.

  Jackob Massawe (kulia) msimu uliopita alikuwa mchezaji wa Ndanda FC

  Aidha, nahodha huyo amesema katika kikosi chao kumekuwa na makosa ya katika safu ya mashambulizi na safu ya ulinzi hali iliyosababisha wapoteze nafasi nyingi za kufunga magoli na kuruhusu magoli mengi katika michezo miwili.
  Amesema wachezaji wamekosa umakini na kuwa na tamaa ya kila mmoja kutaka kufunga ndiyo sababu aina ya magoli waliyofungwa katika michezo yote yanafanana. Hata hivyo, amesema yeye kama Nahodha na Kocha wao watajitahidi kuhakikisha makosa hayajirudii katika michezo inayofuata.
  “Mchezo na Yanga goli la kwanza tumefungwa dakika za mwanzo za mchezo na dakika za mwishoni za mchezo za kipindi cha kwanza ambazo ukitizama ni sawa na dakika tulizofungwa dhidi ya KMC tumeruhusu magoli mengi kwa kuwa umakini katika safu ya ulinzi ni mdogo,”.
  “Mimi kama nahodha wa kikosi na Kocha wangu tutajaribu kuzungumza na wachezaji kuhakiksha makosa hayajirudii lakini pia kocha ameutizama vizuri michezo yeye kama mwalimu  ameona makosa yalipo sidhani kama michezo ijayo haya mambo yatajirudia,”alisema Massawe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAHODHA WA STAND UNITED AWAAMBIA NDANDA FC; “TUMEWASOMA, JIPANGENI TUNAKUJA KWA HASIRA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top