• HABARI MPYA

  Monday, September 24, 2018

  MTIBWA SUGAR WAWATANDIKA AFRICAN LYON 2-0 UHURU, MABAO YOTE AMEFUNGA JAFFAR KIBAYA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  MABAO ya mshambuliaji chipukizi, Jaffar Kibaya yameipa ushindi wa 2-0 Mtibwa Sugar katika mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu ya Tanzania Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo.
  Kibaya alifunga mabao yake yote kipindi cha kwanza, la kwanza dakika ya 30 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenza, Stahmili Mbonde na la pili dakika ya 35 akiunganisha krosi ya kiungo Salum Kihimbwa.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi sita, wakati Lyon inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi sita pia.

  Jaffar Kibaya (kulia) amefunga mabao yote Mtibwa Sugar ikishinda 2-0 leo

  Kikosi cha African Lyon kilikuwa: Tonny Charles, Khalfan Mbaruku, Omary Salum/Kassim Mdoe dk46, Agustino Samson, Daud Salum, Said Mtikila, Awadh Salum, Ismail Adam, Haruna Moshi ‘Boban’, Victor Da Costa/Kassim Alimbwe dk82 na Adam Omary. 
  Mtibwa Sugar: Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Dickson Daudi, Hassan Isihaka, Shaaban Nditi, Ismail Mhesa, Ally Yussuph, Jaffar Kibaya/Hussein Javu dk89, Stahmili Mbonde/Henry Joseph dk73 na Salum Kihimbwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAWATANDIKA AFRICAN LYON 2-0 UHURU, MABAO YOTE AMEFUNGA JAFFAR KIBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top