• HABARI MPYA

  Saturday, September 29, 2018

  SAMATTA NI BALAA, NA LEO AMAPIGA HAT TRICK TENA KRC GENK YASHINDA 4-0 LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo amefunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa mabao 4-0 wa KRC Genk dhidi ya Zulte-Waregem katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena.
  Samatta alifunga mabao yake katika dakika za 31, 67 na 86 wakati bao lingine la Genk limefungwa na kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 29.
  Hiyo ni hat trick ya pili kihistoria kwa Samatta tangu ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

  Mbwana Samatta na leo amefunga hat trick KRC Genk ikishinda 4-0 dhidi ya Zulte-Waregem 

  Na kwa ujumla, Samatta tangu ametua Genk amekwishacheza jumla ya mechi 120 za mashindano yote na kufunga mabao 46.
  Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 94 na kufunga mabao 32, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 18 mabao 12.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Dewaest, Aidoo, Maehle, Berge/Heynen dk82, Malinovskyi, Pozuelo/Seck dk74, Trossard, Ndongala/Paintsil dk71 na Samatta.
  Zulte-Waregem; Bossut, the Fauw, Baudry, Marcq/Heylen dk45, Buffalo/Soisalo dk85, Faik, De Pauw/Bedia dk45, Walsh, Demir, Sylla na Bjordal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA NI BALAA, NA LEO AMAPIGA HAT TRICK TENA KRC GENK YASHINDA 4-0 LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top