• HABARI MPYA

  Monday, September 24, 2018

  MBAO FC YAIPIGA PRISONS 1-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU, NDANDA FC WAPIGWA 3-1 NA STAND NANGWANDA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Mbao FC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa CCM Kirumba mjini  Mwanza.
  Ushindi huo umetokana na bao la Robert Ndaki dakika ya 90 na ushei akitumia makosa ya safu ya ulinzi timu ya timu ya Jeshi la Magereza Tanzania.
  Kwa ushindi huo, Mbao FC inayofundishwa na beki wa zamani wa Simba SC, Amri Said ‘Stam’ inafikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi sita, ikizishusha Yanga SC yenye pointi 12 za mechi nne, Azam FC yenye pointi 11 na Simba SC yenye poinyi za mechi tano kila moja.

  Robert Ndaki amefunga bao pekee dakika ya mwisho Mbao FC ikiichapa Prisos  1-0

  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, timu nyingine ya Kanda ya Ziwa, Stand United imeng’ara kwa ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Sixtus Sabilo aliifungia Stand United ‘Chama la Wana’ bao la kwanza dakika ya 37, kabla ya Bigirimana Blaise kufunga mawili dakika za 53 na 82 na Ismail Mussa kuifungia bao la kufutia machozi Ndanda dakika ya 90 na ushei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBAO FC YAIPIGA PRISONS 1-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU, NDANDA FC WAPIGWA 3-1 NA STAND NANGWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top