• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2018

  MBEYA CITY WAPANIA KUMALIZIA HASIRA ZAO KWA STAND UNITED KESHO SHINYANGA

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mbeya city kesho itashuka dimbani kumenyana na timu ya Stand United katika mji wa Shinyanga ikiwa ni mchezo wao wa nane, Mbeya City wameshinda michezo miwili, wakitoka sare mchezo mmoja nakupoteza michezo minne.
  Afisa habari wa timu hiyo Shah Mjanja amesema mchezo wao wa kesho ni mahususi kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu ambazo zitawatoa katika nafasi ya chini walioyopo katika msimamo wa ligi.
  “Tulianza ligi vizuri tukitumia uwanja wetu wa nyumbani lakini mambo yalibadilika, tunajua ligi hii ni ngumu lakini tutajitahidi kesho kupata ushindi wa mapema ili tutoke katika nafasi tuliyopo”. Amesema Shah.

  Mbeya City ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu kati ya timu 20 zinazoshiriki, ikiwa na jumla ya alama 7, mchezo wa mwisho walicheza na Singida United katika uwanja wa Namfua uliopo Mkoani Singida, Mbeya City alipoteza mchezo huo kwa kukubali kichapo cha magoli 3-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAPANIA KUMALIZIA HASIRA ZAO KWA STAND UNITED KESHO SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top