KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depú’ (26) kuwa mchezaji wake mpya akitokea Radomiak Radom ya Poland.
Depu alivuta hisia za viongozi wa Yanga baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) akifunga mabao manane Juni mwaka jana Jijini Bloemfontein, Afrika Kusini akiiwezesha Angola kutwaa taji hilo kwa mara ya tano.
Kisoka Depu aliibukia kituo cha soka ya vijana cha Electro do Lobito mwaka 2017 kilichopika vipaji vingi Angola.
Baadaye alichezea klabu za Académica Lobito, Recreativo Caála, Sagrada Esperança na Petro de Luanda zote za Angola kabla ya kwenda Ureno kuchezea Gil Vicente mwaka 2023, ambayo mwaka jana ilimpeleka kwa mkopo Vojvodina ya Serbia kumalizia mkataba wake wa miaka miwili.
Juni 30 mwaka jana baada ya kung’ara kwenye COSAFA, mchezaji huyo alisaini mkataba miaka mitatu kujiunga na Radomiak Radom ya Poland - ambao kabla haujamalizika anahamia Yanga SC.
Amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Angola tangu mwaka 2021.



.png)
0 comments:
Post a Comment