• HABARI MPYA

  Wednesday, September 26, 2018

  SIMBA SC KUINGIA KAMBINI LEO KUNDUCHI MAANDALIZI MECHI NA YANGA, MAZOEZI BOKO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Simba SC inatarajiwa kuingia kambini leo katika hoteli ya Sea Scape, Kunduchi mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumapili dhidi ya mahasimu, Yanga SC.
  Uongozi wa Simba SC chini ya Rais wake, Salum Abdallah ‘Try Again’ ulipenda sana kuipeleka timu Zanzibar kama ilivyo kawaida, lakini kocha Mbelgiji Patrick J. Aussems amekataa hilo akisema ni kuwasumbua wachezaji.
  Baada ya mapumziko ya siku moja timu ikirejea kutoka Kanda ya Ziwa kwa mechi nyingine za Ligi Kuu, SImba SC inatarajiwa kuendelea na mazoezi leo Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya mji.

  Yanga SC waliondoka juzi kwenda mjini Morogoro kuweka kambi kujiandaa na mchezo huo, ikiwa ni siku moja tu baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa.
  Huo ulikuwa ushindi wa nne mfululizo katika mechi zote nne za mwazo za Ligi Kuu, baada ya awali kushinda 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, 4-3 dhidi ya Stand United na 1-0 dhidi ya Coastal Union, zote Uwanja wa Taifa.  
  Ikumbukwe Simba SC wataingia kwenye mchezo huo wakitoka kucheza mechi tano, wameshinda tatu 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa na 3-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, sare moja 0-0 na Ndanda FC mjini Mtwara na kufungwa moja, 1-0 na Mbao FC huko Mwanza.
  Huo utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo mwaka huu, baada ya Aprili 29 Simba SC kushinda 1-0, bao pekee la Erasto Edward Nyoni dakika ya 37, mechi ya marudiano ya msimu uliopita wa Ligi Kuu. 
  Mechi ya kwanza ya msimu huo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Oktoba 28 Uwanja wa Taifa Simba wakitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57, kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUINGIA KAMBINI LEO KUNDUCHI MAANDALIZI MECHI NA YANGA, MAZOEZI BOKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top