• HABARI MPYA

  Friday, September 21, 2018

  YANGA SC KUMKOSA KELVIN YONDAN MECHI NA SINGIDA UNITED JUMAPILI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itamkosa beki wake, Kelvin Yondan katika mchezo wa Jumapili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Singida United kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
  Yondan ameweka rekodi msimu huu baada ya kuonyeshwa kadi tatu mfululizo katika mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, Stand United na Coastal Union.
  Lakini habari njema kwenye kikosi cha Yanga ni kurejea kwa beki wa pembeni, Juma Abdul aliyekosekana kwenye mechi mbili zilizopita kwa sababu ya maumivu.
  Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi leo Uwanja wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Polisi, Kurasini mjini Dar es Salaam baada ya mapumziko ya siku moja kufuatia mechi ya Jumatano dhidi ya Coastal Uwanja wa Taifa.

  Kelvin Yondan atakosekana katika mchezo dhidi ya Singida United kwa sababu ya kadi tatu za njano

  Daktari wa Yanga SC, Edward Bavu amesema kwamba hakuna majeruhi kwenye timu zaidi ya viungo Juma Mahadhi na Baruwan Akilimali ambao tayari wameanza mazoezi mepesi.
  Adha, wachezaji beki Mwinyi Hajji Mngwali na viungo Pius Buswita na Said Juma ‘Makapu’ waliokuwa wamesimamishwa kwa utovu wa nidhamu wamerejea mazoezini leo baada ya kuomba radhi na watakuwa sehemu ya wachezaji watakaoingia kambini kuelekea mchezo wa Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUMKOSA KELVIN YONDAN MECHI NA SINGIDA UNITED JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top