• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2018

  CAF YAITHIBITISHA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA FAINALI ZA AFCON 17 MWAKANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeithibitisha rasmi Tanzania kuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa 17 mwakani.
  Hiyo ni baada ya kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utendaji ya CAF kilichofanyika mjini Sharm El Sheikh nchini Misri.
  Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema jana mjini Dar es Salaam kwamba tayari CAF imetuma barua ya kuithibitisha Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON U17 mwakani.

  “Na hapa nyumbani maandalizi yanaendelea vizuri tu, kwa maana ya maandalizi ya mashindano yenyewe, lakini kuiandaa timu kuelekea kwenye mashindano hayo,”alisema Ndimbo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAITHIBITISHA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA FAINALI ZA AFCON 17 MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top