KLABU ya Azam FC imemtoa kwa mkopo winga wake Mtunisia, Baraket Hmidi kwenda Diyala SC ya Iraq hadi mwisho mwa msimu.
Taarifa ya Azam FC Kuhusu winga huyo wa kulia usiku huu imesema; “Azam FC inathibitisha kwamba, Baraket Hmidi, amejiunga na klabu ya Diyala SC ya Iraq kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu huu. Tunamtakia kila kheri katika kipindi chote atakachokuwa huko,”.
Baraket Hmidi aliwasili Azam FC Agosti mwaka jana akitokea CS Sfaxien alikodumu tangu mwaka 2022 baada ya kusajiliwa kutoka Stade Gabèsien, zote za kwao, Tunisia.



.png)
0 comments:
Post a Comment