• HABARI MPYA

  Saturday, September 22, 2018

  MAN UTD YALAZIMISHWA SARE NA WOLVES 1-1 OLD TRAFFORD

  Wachezaji wa Manchester United wakirejea katikati kinyonge baada ya Wolves kusawazisha bao katika sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford leo. United walitangulia kwa bao la mchezaji wake mpya, kiungo Frederico Rodrigues Santos 'Fred' dakika ya 18 akimalizia pasi ya Mfaransa Paul Pogba, kabla ya Joao Moutinho kuisawazishia Wolverhampton dakika ya 53 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mmexico, Raul Jimenez. Mchezo huo ulihudhuriwa na kocha wa zamani wa Mashetani Wekundu, Sir Alex Ferguson kwa mara ya kwanza tangu aripotiwe kuugua Mei mwaka huu 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UTD YALAZIMISHWA SARE NA WOLVES 1-1 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top